December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Saratani ya mlango wa kizazi inachangia asilimia 36 ya vifo vitokanavyo na saratani

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

IMEELEZWA kuwa saratani ya mlango wa kizazi(HPV) inachangia kwa takribani asilimia 36 ya vifo vyote vitokanavyo na saratani za maeneo mengine.

Ambapo takribani watu milioni 10 kila mwaka wagonjwa wapya wanapatikana na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo kati ya hao milioni 6 hupoteza maisha kila mwaka Afrika.

Hayo yameelezwa jijini hapa leo,Aprili 12,2024 na Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya ,Dkt.Lotalisi Gadau wakati akitoa semina kwa waandishi wa habari kuhusu kampeni ya uhamisishaji wa chanjo dhidi ya mlango wa kizazi nchini ambayo inawahusu mabinti wa umri kuanzia miaka 9 hadi 14 kuelekea maadhimisho ya wiki ya chanjo Aprili 22 hadi 28 mwaka huu nchini.

Amesema kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wa sqratani ya mlango wa kizazi nchini wanafika hospitali kupata matibabu upelekwa wakiwa wamechelewa na hivyo wengi hupoteza maisha.

Gadau ameeleza kuwa kutokana na hayo Serikali imeona tatizo ni kubwa hivyo ikaona haiwezi ikafumbia macho na kuhakikisha kwamba inaweka hafua ya kwamba inatoa chanjo ilikuweza kuwakinga wanawake nchini ili wasipoze maisha kila mwaka kwa saratani ya mlango wa kizazi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Kinga kutoka Wizara ya Afya,Dkt.Tumaini Haonga amesema kuwa Wizara ya afya imebaini muitikio mdogo kwa dozi ya pili ya chanjo ya mlango wa kizazi hivyo inakwenda kutoa dozi moja ambayo inajitosheleza.

Dkt.Tumaini amesema kuwa wiki ya chanjo inalenga msisitizo wa kutoa elimu ,kuhamasisha na kuongeza muitikio wa jamii kuhusu chanjo zinazotolewa dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo

“Tumeona ni fursa muhimu kuitumia wiki hii katika kuelimisha kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi,tunafanya hivyo kwasababu kubwa mbili,chanjo ya HPV imeendelea kutolewa nchini kwa kipindi kirefu sasa na wakati huu tumebaini muitikio mdogo wa hususan katika dozi ya pili ya chanjo kwani utaratibu wa mwanzo chanjo ya kwanza na ya pili tulikuwa tunatoa kwa watoto,mabinti wenye umri wa miaka 14 na wengi tulikuwa tunawapata wakiwa shuleni.

“Kama tunavyofahamu sera za elimu watoto wanaanza darasa la kwanza wakiwa na miaka 7 kwahiyo miaka 14 tulikuwa tunampata akiwa darasa la saba au kidato cha kwanza ,Kwahiyo kulikuwa kuna namna tunawakosa akitoka shule ya msingi kwenda sekondari,”amesemq Dkt.Tumaini.

Ameeleza kuwa tafiti ambazo zimeendelea kufanyika duniani,ufuatiliaji ambao umeendelea kufanyika kupitia shirika la afya duniani imeeleza kuwa chanjo hii HPV inaweza kuwa na ufanisi wa kumkinga anayepata chanjo hiyo dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi hata kama akipata dozi moja.

“Dozi moja ya chanjo hii ya saratani hii ya mlango wa kizazi inaweza kumfanya mtu anayepewa chanjo hii inamkinga kimwili dhidi ya saratani ya mlango wa kizazi kwa vigezo ambavyo vimeruhusiwa na shirika la afya duniani lakini na wizara ya afya.

“Sasa kwa msingi huo huo tunakuja na utaratibu wa kuanza kutoa chanjo hii kwa dozi moja,mwanzoni tulikuwa tunamuitikio hafifu lakini pia sasa hivi tunafursa yakutoa dozi moja ambayo ni toshelevu kupata kinga kamili,”amesema.

Vilevile Dkt.Tumaini ameeleza kuhusu ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ambapo amesema ni kama saratani nyingine siyo rahisi kwa mwananchi wa kawaida kuona dalili katika hatua za awali pasipo kufanyiwa uchunguzi .

Amesema kwenye hatua ya pili ndiyo dalili zinaanza kujionesha ambayo mtaalamu wa afya pekee ambaye amepata mafunzo ya afya ndiyo anaweza kubaini na ndiyo ambayo wataalamu wa afya wanaitumia kama fursa ya kufanya uchunguzi wa uwepo wa viashiria vya saratani ya malango wa kizazi kuona kama kuna uharibifu wowote uliojitokeza.

Hatua ya tatu ndiyo dalili za wazi zinaweza kujionesha na hatua ya nne ni ugonjwa kuanza kuhama kwenye via vya uzazi kwenda maeneo mengine ambapo hatua ya tatu na ya nne zote zinachangamoto kubwa ambapo Sehemu kubwa ya matibabu ni huduma ya mionzi na huduma zingine ambazo pia ufanisi mkubwa lakini siyo kwa asilimia 100.

“Hivyo basi tunaweka msisitizo mkubwa kwa wananchi kutumia nafasi ya hatua mbili za kwanza ni hatua ambazo mtu hana dalili zozote za ugonjwa,hatua ambayo mtu hana maambukizi ya virusi na maambukizi haya kwa sehemu kubwa yanaambukizwa kwa tendo la kujaamiana hivyo ni muhimu binti ambaye hajaanza kujishughulisha na kitendo cha kujamiiana aanze kupata fursa ya kupewa kinga iliikitokea amepata maambukizi basi chanjo aliyopewa imsaidie .

“Kwahiyo tuchokifanya chanjo ya HPV ni kuupa mwili kinga imara na nguvu ya kudhibiti maambukizi ya virusi ili mabinti walengwa wasije wakapata athari za maambikizi umri unavyoenda mbele.