June 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sangara ahamasisha daftari la Mpiga kura

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa SANGARA iliyopo Mvuti kata ya Msongola wilayani Ilala, Pili Ndimanya, ameamasisha wananchi wajiandikishe katika Daftari la mpiga kura Mwezi Julai mwaka huu.

Mwenyekiti Pili Ndimanya , alisema hayo katika mkutano wa hadhara wa wananchi wa mtaa huo wakati wa kuelezea utekelezaji wa Ilani na kupokea kero za wananchi.

“Wananchi wangu wa Mtaa wa SANGARA nawaomba mwezi Julai mshiriki katika daftari la Mpiga kura ili muweze kupata haki ya msingi ya kupiga kula katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka huu 2024″alisema Pili .

Mwenyekiti pili aliwataka Wazazi wa Sangara kuwamasisha pia watoto wao waliotimiza miaka 18 pamoja na wageni wanaohamia eneo hilo ili waweze kupata fursa ya kupiga kura lazima wawe katika daftari hilo.

Alisema kupiga kura ni Demokrasia ya kila mmoja kwa ajili ya kuchagua viongozi wa Serikali ili waweze kuingia madarakani kuongoza dola na kutumikia wananchi.

Aidha pia katika mkutano huo wa wananchi kuliibua Changamoto za Urasimishaji ARDHI wananchi wengi maeneo yao bado kurasimisha ardhi,pamoja na Changamoto ya masuala ya Ulinzi na Usalama eneo hilo bado wananchi kuanza kulinda Polisi Shirikishi .

Mwenyekiti Pili pia alisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ana mikakati ya kujenga shule hivi karibuni kuondoa adha ya wanafunzi kwenda kusoma shule za mbali.

Mjumbe wa Mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa Dar es Salaam Thomas Nyanduli, alielezea Utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM kata ya Msongola uliofanyika na Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan na kusimamia miradi hiyo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa na Diwani wake wa Kata ya Msongola AZIZI MWALILE ambapo alisema Dkt Samia Suluhu Hassan anajenga kituo cha afya cha kisasa Mvuti ambapo kinagharimu zaidi ya shilingi milioni 500.

Aliwataka wakazi wa Mvuti Sangara kuendelea kuwamini watekelezaji wa Ilani na kuwaunga mkono katika kusimamia miradi ya maendeleo ya sekta ya afya na sekta ya Elimu .

Pia alisema Serikali ipo hatua za Mwisho eneo la SANGARA kujenga chuo cha Ufundi cha wilaya ya Ilala kutakachotumiwa na wanafunzi mbalimbali hivyo wawe wavumilivu matunda ya Serikali yanakuja hivi karibuni Msongola itakuwa ya kisasa.