January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia kama Star India

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ziara ya Rais Samia nchini India imetamba katika vyombo vya habari kuanzia magazeti mpaka mitandaoni.

Rais Samia amemaliza ziara ya kitaifa ya siku nne nchini India ambayo imekuja siku chache baada ya taifa hilo kuandaa mkutano wa nchi tajiri duniani wa G20.

Ziara hiyo ilipata umaarufu kiasi kwamba jina lake likawa namba mbili miongoni mwa majina yaliyosomwa sana mtandaoni nchini India kwa mujibu wa mtandao wa Google.

Habari kubwa zilizoandikwa zaidi na magazeti zilizungumzia kuhusu mahusiano ya Kihistoria baina ya nchi hizo na pongezi za Afrika kwa India kutokana na kuipigania kuingia kuwa mwanachama wa G20 kupitia Umoja wa Afrika.