Na Penina Malundo, Timesmajira Online
CHAMA cha Wataalamu na Wanataaluma wa Ustawi wa Jamii Tanzania(TASWO),kimempongeza Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha nia na umuhimu wa kuitenganisha Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii na Afya kuwa idara ya kujitengemea kwani idara hiyo imebeba majukumu makubwa ambayo utekelezaji,ufuatiliaji ,usimamizi na uratibu wake ulikuwa na changamoto katika kuwafikishia huduma bora za ustawi wa jamiii wa wananchi.
Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Chama cha TASWO, Awadh Mohamed wakati akiongea na waandishi wa habari amesema kupitia hotuba aliyetoa Rais Samia Disemba 16,2021wakati wa uzinduzi wa kamati ya Ushauri ya Kitaifa Kuhusu Utekelezaji wa ahadi za nchi kwenye jukwaa la kizazi chenye usawa.
Mohamed amesema utenganishaji wa idara kuu hiyo ni jambo muhimu na lenye tija katika jamii katika kuwafikia wananchi wake hususani makundi maalum na watu wenye uhitaji maalum ambapo awali ilikuwa ni ngumu kufikia makundi hayo na kukosa kizazi chenye usawa .
“Katika kufanikisha malengo mazuri ya Rais Samia ikiwepo kuwepo kwa kizazi chenye usawa kama sehemu ya Tanzania kutekeleza lengo la maendeleo endelevu kidubia na kuboresha huduma za ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii nchini,”amesema na kuongeza
“Katika idara kuu ya Maendeleo ya Janii kwenye awamu ya sasa,kumekuwepo na majukumu mengi zaidi mbali na Afya ikiwemo huduma za ustawi wa Jamii ambazo ni kubwa kwa majukumu yake,”amesema
Mohamed amesema huduma za ustawi wa jamii zimekuwa ni huduma mtambuka toka uhuru na kuwa muhimu katika kuzuia matatizo ya kijamiii yanayoweza kuathiri jamii na hasa makundi maalum.
Ametaja makundi ambayo yamekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za msaada wa kisaikolojia na kijamii kuanzia ngazi ya mtu mmoja hadi familia ni pamoja na kundi la wanawake , wasichana watoto yatima,watoto wa mitaani ,watoto wanaokinzana na sheria ,watoto walio katika mazingira hatarishi,watu wenye ulemavu,wazee,waathirika wa ukatili na unyanyasaji.
Amesema wataalamu wa ustawi wa Jamii duniani wamepewa wajibubwa kushughulika na makundi maalum kwa sababu utoaji wa huduma hizo unaongozwa na maadili ,misingi na miiko ya taaluma yao kama ilivyo kwa kada za afya.”kutokana na umuhimu na ukubwa wa huduma zinazotolewa na sekta ya ustawi wa jamii,nchi mbalimbali zimeweka wizara kamili kama sio maalum au idara kuu kuanzia ngazi ya Taifa hadi Serikali za mitaa ili kuweza kupanga,kuratibu na kutekeleza huduma na hafua mbalimbali kuwafikia wahitaji wote,”amesema
Mohamed amesema kwa miaka mingi sekta ya ustawi wa jamii nchini haijapata nafasi inayostahili kimuundo na hivyo kuathiri huduma za ustawi wa jamii kwa makundi yote yaliyotajwa licha ya kuwa na sera, sheria na miongozo mbalimbali inayoongoza utoaji wa huduma hizo.
“Kutokuwa na Idara kamili ya Ustawi wa jamii katika ngazi ya Halmashauri, imepelekea kukosa kifungu maalumu cha kupangiwa bajeti ya kutosha pia kutokuwepo na idara hiyo kamili imekuwepo changamoto ya kuwasilisha masuala ya ustawi wa Jamii kwenye timu ya menejementi ya halmashauri kwa ukamilifu na hivyo kukosa kutetea mipango kwa ajili ya kuhudumia makundi tajwa na yenye uhitaji,”amesisitiza na kuongeza
“Kwenye nia hii njema ya Rais Samia ya kutenganisha sekta ya Afya na Idara kuu ya maendeleo ya jamii, ni imani yetu TASWO kama wadau wakuu wa ustawi wa jamii, kuwa huu ni wakati muafaka sasa kwa sekta hii ya Ustawi wa jamii kupewa uzito wa pekee kuanzia ngazi ya Taifa hadi mamlaka za serikali za Mitaa na hivyo kujenga kizazi chenye usawa kama yaliyvyo malengo ya Rais Samia na malengo ya Dunia,”amesema
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa