Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dar
RAIS Samia Suluhu Hassan, amesikia kilio cha watumishi kuhusu kikokotoo, ambapo mabadiliko ya kikokotoo yalishusha kundi la wafanyakazi waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50 mpaka asilimia 33 na kundi waliokuwa wakipokea asilimia 25 walipandishwa mpaka asilimia 33.
Kufuatia kilio hicho, Rais Samia imesikia kilio hicho na amekifanyia kazi kwa maslahi mapana ya wastaafu wetu na wanaotarajiwa kustaafu.
Hayo yamesemwa Bungeni jijini Dodoma Juni 3, 2024 na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2024/2025.
“Rais Samia ameelekeza kuongezwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo sasa hadi asilimia 40.
Hili ndio kundi kubwa la watumishi wanaofanya kazi nzuri sana kwa taifa letu wakiwepo, walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi mengine yalioko Serikali kuu na Serikali za Mitaa,” amesema.
Alisema Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33 sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu.
“Watumishi takriban 17 walioathirika na mabadiliko haya watazingatiwa katika mabadiliko haya. Serikali itaendelea kuangalia maslahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko,” amesema.
Amesema mafanikio hayo yote yamepatikana chini ya uongozi mahiri na thabiti wa Dkt. Samia
“Hii inadhihirisha kuwa Mama anawapenda sana Watanzania, hivyo basi na sisi Watanzania Tusimame na MAMA kwa kumpatia wasaidizi makini kutoka Chama Cha Mapinduzi watakaoendeleza gurudumu la maendeleo kupitia uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 2024.” Amesema.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua