November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Samia aandika rekodi uzalishaji wa Sukari

-Waongezeka kwa zaidi ya tani 70,000 mwaka 2022/23

-Akiba kwenye maghala nayo yapaa, Waziri wa Viwanda aanika siri ya mafanikio

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia SuluhuHassan, imevunja rekodi ya uzalishaji wa sukari ambapo kati ya mwaka2022-2023 uzalishaji umeongezeka kwa zaidi ya tani 70,000.

Aidha akiba ya sukari iliyopo katika maghala hadi sasa ni zaidi ya tani 170,000.Matokeo ya ongezeko kubwa la sukari nchini imeelezwa kuwa ni jitihadazinazofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Samia kwa kuhamasisha uzalishajina uwekezaji katika tasnia hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji, wakati wa kikao na wadau wauzalishaji wa sukari chenye lengo la kupata hali ya uzalishaji wasukari nchini, katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Dkt.Hashil Abdalah alisema wanaendelea kuhakikisha kuwa uwekezajiunakuwepo na unakuwa na tija kwa Taifa zima.

“Katika kikao chetu tumegundua kuwa sekta ya sukari imeshafanyaupanuzi mkubwa na imeshaimarika kwa kiwango kikubwa sana kwenye nchiyetu kiasi kwamba uzalishaji wa sukari umeongezeka kwa Kiwangokikubwa”

“Mwaka huu tumeingiza uzalishaji wa sukari wa kiwanda kipya Bagamoyoambao umepelekea uzalishaji wa sukari kwa ujumla wake mwaka huu kuwani mkubwa zaidi kuliko hata ule wa mwaka jana, hii inapelekeamazungumzo haya kuendelea mara kwa mara,” aliongeza Dkt. Hashil.

Rais Samia mara kadhaa amekuwa akiweka wazi kuwa Tanzania inawahitajizaidi wawekezaji kuliko wao wanavyohitaji kuwekaza katika nchi hii.

Hivyo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imejipanga kuwa nasera ambazo zinaonesha miaka ijayo kutakuwa na jambo gani nchini,kuchukua hatua za haraka, madhubuti na za uhakika kuhakikishauwekezaji unaimarika.Kuhakikisha bidhaa zinapatikana kwa wakati lakini pia kuhakikishaajira hasa za Watanzania zinazalishwa kutokana na uzalishajimbalimbali.

Pia kutokana na jitihada zinazofanywa na wawekezaji kwenye sekta yasukari Dkt. Hashil aliwahakikishia wakulima hasa wale wa miwa kiliochao cha kupata masoko ya miwa kimekwenda kutatuka, kama ambavyowameweza kuingiza tani 70, 000 nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Sera na Mipango wa Wizara yaKilimo, Gungu Mibavu, alisema kutokana na ongezeko la uzalishaji wasukari nchini, inaonesha kwamba jitihada zinazofanywa na serikali yaawamu ya sita katika kuhamisha uzalishaji na uwekezaji katika tasniahiyo zimeendelea kuzaa matunda hivyo ameipongeza serikali ya awamusita katika eneo hilo.

“Kumeonekana kuna uchechemuzi wa uwekezaji na uzalishaji wa sukarikatika tasnia hii kwa mwaka huu ukilinganisha na miaka mingineiliyopita”.

Naye Mwenyekiti wa chama cha wazalishaji wa sukari Tanzania, Seif.Seif, aliiomba Serikali na wadau mbalimbali kutoa ushirikiano wakuhakikisha ajira zinatolewa lakini pia dhamana ya kukuza uchumi wandani iweze kuendelea.