November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sakata la machinjio vingunguti SUA Madiwani Ilala waliamsha

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo wametaka waelezwe lini mradi wa machinjio ya kisasa VINGUNGUTI yanafunguliwa rasmi .

MADIWANI hao wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walitoa hoja hiyo Katika kikao cha Baraza la Madiwani katika maswali ya papo kwa papo ambapo hoja hiyo iliungwa mkono na madiwani wote.

Akizungumza katika Baraza hilo Mbunge wa Viti Maalum Janeth Masaburi alisema ujenzi wa mradi wa machinjio ya VINGUNGUTI Kila siku unasua hatima yake bado kufamika tunaomba tuelezwe ukweli ikishindikana tuombe Serikali Kuu itusaidie.

“Tunaomba tuelezwe ukweli kusuasua kuanza kazi ya kufunguliwa Machinjio ya kisasa VINGUNGUTI tujue unamalizika lini mradi huu mkubwa wa Serikali mda wake ulitakiwa ukabidhiwe umepita mpaka leo kimya “alisema Masaburi.

Mbunge Masaburi aliomba miradi huo ukabidhiwe pamoja na miradi mingine yote imalizike kwa wakati kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mwanamke Samia Suluhu Hassan katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.

Katika Baraza hilo Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam waliunga mkono hoja hiyo kufatilia Maendeleo ya miradi ya Machinjio wakitaka Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na Meya kuchukua hatua kufatilia kujua ujenzi huo umekwama kwanini mpaka sasa ujafunguliwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu alisema Kikao Cha Kamati ya fedha na Utawala na kutoa maelekezo ndani ya miezi mitatu machinjio hayo yawe yamefunguliwa.

Tabu Shaibu alisema miezi mitatu hiyo inaanza mwezi Machi mwaka huu hadi Mei mwaka huu yatakuwa yamemalizika.

Mbunge wa Viti Maalum Janeth Masaburi akizumza Katika kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Machi 02./2022 katika Kikao hicho Mbunge Masaburi aliuliza kuhusu kusua sua kufunguliwa Machinjio ya kisasa VINGUNGUTI Wilayani Ilala (PICHA NA HERI SHAABAN)
NAIBU MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Sady Kimji akisoma taarifa ya Kamati ya fedha na Utawala Katika kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Machi 02/2022(PICHA NA HERI SHAABAN)
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam IMELDA SAMJELA na Tumike Malilo wakiwa katika kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam leo Machi 02/2022(PICHA NA HERI SHAABAN)
Mwenyekiti wa Kamati za Huduma za Jamii Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Steven Mushi, akiwasilisha Taarifa za Kamati yake Katika kikao Cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Jiji leo Machi 02 mwaka ( huu PICHA NA HERI SHAABAN)