Na Bakari Lulela,Timesmajira
MW,ENYEKITI wa serikali ya mitaa wa Mkunduge Tandale jijini Dar es salaam, Said Mrisho Said akifuatilia hatua ya uboreshaji wa miundombinu korofi kutoka kwa mafundi wa Dawasa ambayo ni aidha kubwa kwa wananchi kwenye upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama.
Hatua hiyo ilikuja baada ya mwenyekiti huyo kufanya ziara kwenye vyanzo vya mito vinavyotoa huduma ya usambazaji wa maji maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam na Pwani ukosefu wa upatikanaji wa huduma hiyo kwa muda mrefu mahala hapo ilipelekea wananchi kuhangaika kuitafuta usiku na mchana, hali iliyopelekea ndoa nyingi kuingia dosari.
Akizungumza baada ya kufika maeneo korofi, mwenyekiti huyo amesema kuwa ipo haja ya kufanya ukagizi wa mara kwa mara kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji kwa wakaazi wa maeneo hayo.

“Changamoto ya ukosefu wa miundombinu ya maji safi na salama kwa wakaazi wangu wa Mkunduge imetokana na ukuu wa mbomba ambapo kwa sasa tumefanya maboresho kwa kuwatumia mafundi wazoefu kutoka mamlaka ya maji safi (DAWASA),” amesema Said
Aidha Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa kutokana na maboresho hayo amewahakikishia wakaazi wake wa Mkunduge kuwa changamoto ya ukosefu wa maji sasa itakuwa ni historia kwenye eneo hilo.
Hata hivyo mkuu huyo amewataka wananchi wake kuwa makini na watu waovu wasiopenda maendeleo ya serikali ya awamu ya sita hutokea kuharibu kwa makusudi miundombinu sahihi vya maji safi kwa kuwatolea taarifa ama kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
More Stories
TAKUKURU Gairo waja na kliniki tembezi kutoa elimu ya kupambana na Rushwa
Wadau wakutana kwa tathimini maendeleo ya Elimu
JKCI:Tiba Mkoba ya Dkt.Samia yawafikia watu 21,324