Na Yusuph Mussa,Timesmajiraonline,Kilindi
WAKALA wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, inatarajia kutumia sh. bilioni 4,734,148,603 kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Katika fedha hizo,sh.2,275,354,840 ni kutoka Serikali Kuu na Mfuko wa Maji wa Taifa, na fedha za wafadhili ni sh. 2,458,793,763. Katika bajeti hiyo, sh. 4,117,074,018 ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, na sh. 617,074,585 kwa ajili ya uendekevu wa miradi, utafiti, usanifu na uendeshaji wa ofisi.
Hayo yamesemwa leo Januari 29, 2025 na Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kilindi Mhandisi Philipo Bajuta wakati anawasilisha bajeti hiyo kwenye Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, na kuitaja miradi itakayotekelezwa kutokana na fedha hizo.
Mhandisi Bajuta amesema Wilaya ya Kilindi inategemea kuendelea na ukamilishaji wa miradi ya maji inayoendelea kujengwa kupitia fedha za Mfuko wa Maji yenye thamani ya sh. 33,811,048,693, na kuitaja miradi hiyo kuwa ni Mradi wa Maji Kwamaligwa/Gitu sh. 6,988,881,532
Mingine ni Mradi wa Maji Diburuma/Songe sh. 22,956,445,680, ujenzi wa Mradi wa Bwawa Saunyi (Lombout) sh. 3,392,406,481, na Uchimbaji wa Visima 19 katika vijiji 19 sh. 473,315,000.
Mhandisi Bajuta amesema wilaya hiyo pia inategemea kuendelea kutekeleza miradi mipya ya maji kupitia fedha za Mfuko wa Maji (NWF) na Serikali Kuu (GoT) yenye thamani ya sh. 11,604,494,473 ambayo ni ujenzi wa Bwawa la Maji Msente sh. 2,350,460,500.
Mingine ni Mradi wa Maji Kwaluguru/Negero sh. 6,348,584,798, ujenzi wa Bwawa la Maji Mnkonde sh. 2,672,831,000, na upelekaji wa umeme mkubwa wa TANESCO katika vyanzo vya maji vya Balang’a/Jungu, Lwande na Mafulila sh. 232,618,175.
“Wilaya ya Kilindi inategemea kukamilisha ujenzi wa miradi ya maji (inayoendelea) kupitia fedha za wafadhili (PforR) yenye thamani ya sh. 1,388,602,155 ambayo ni upanuzi wa Mradi wa Maji Kikunde/Ludewa sh. 368,630,000, ujenzi wa Mradi wa Maji Mkindi sh. 409,532,155, ujenzi wa Mradi wa Maji Kilindi Asilia/Misufini sh. 383,620,000, na ujenzi wa Point Source (5) katika vijiji vya Msente, Mswaki, Sangeni, Mangidi na Mtonga sh. 176,820,000.
“Wilaya ya Kilindi inategemea kuendelea kutekeleza miradi ya maji (miradi mipya) kupitia fedha za Wafadhili (PforR) yenye thamani ya sh. 703,117,023 ambayo ni miradi midogo midogo ya maji (Point source) katika vijiji 19 kutegemea na ripoti ya uchimbaji. Vijiji hivyo ni Sangeni, Mswaki, Makingo, Kisangasa, Mvungwe, Kwamba, Sambu, Mheza, Ngeze, Mapanga, Makelele, Lumotio, Mzinga, Kimembe, Vunila, Kweisapo, Lukole, Vyadigwa na Kitingi”amesema Mhandisi Bajuta.
More Stories
Manispaa ya Shinyanga yaandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza kwa 99%
TAKUKURU yabaini miradi nane yenye dosari
Ilemela yakusanya bilioni 7, mapato ya ndani