December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ruthberta Suppy yafunguka juu ya umuhimu wa kupanda na kutunza miti nchini

Na David John timesmajia online Geita

MKURUGENZI wa Kampuni ya Ruth Bertha Supply Ruthberta Myonga amesema kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi Kuna umuhimu wa kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki kikamilifu upandaji miti ikiwa pamoja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau wa Mazingira nchini

Hayo yamesemwa leo Septemba 22 Mwaka huu Mkoani Geita na Mkurugenzi wa Ruthberta ,Ruthberta Myonga kwenye Maonyesho ya 6 ya Teknolojia Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Bombambili .ambapo pia ametumia fursa hiyo amewahamasisha wanawake kote nchini kupanda miti ya matunda na kivuli Kwa lengo la kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.

Amesema kuwa mbali na kupanda miti ya matunda pia wajikite katika kupanda miti ya maua na hiyo ni kutokana na Fursa inayopatikana katika miti ya maua ambapo itawasaidia kujikwamua kiuchumi .

” Ruthberta Kampuni tupo katika Maonyesho haya lengo kubwa nikuja kuwahamasisha Watanzania juu ya umuhimu wa kupanda miti na kutunza mazingira na Sasa Kuna changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabia ya nchi hivyo ni muhimu Kwa kila Mtanzania kupanda na kutunza Mazingira kwenye maeneo yanayowazunguka “amesema

Nakuongeza kuwa ” hivi Sasa katika mikoa ya Kanda ya ziwa ikiwemo Mkoa huu wa Geita kumekuwa na muamko mkubwa wa watu kupanda miti ya matunda na hata hapa mmeona watu mbalimbali wanakuja kuuliza na kununua miti kwani wamejua umuhimu wa kupanda miti nakwamba tunahamasisha zaidi kupanda miti ya matunda ,miti dawa, na miti ya kivuli.” Amesisitiza

Ruthberta pia ametoa shukrani zake Kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wadau ikiwa pamoja na kutoa matamko mbalimbali yanayohamasisha upandaji wa miti na kupitia Kampuni yake watahakikisha wanaongeza kasi ya kuelimisha Watanzania pamoja na kuzalisha miti Kwa wingi ili kila Mwananchi apande miti hiyo .

Ameongeza kuwa wao kama Kampuni licha ya kuwataka Watanzania kupanda miti lakini pia wanahakikisha wanafuatili ili kupata taarifa zake Kwa lengo la kuona miaka 200 ijayo itakuwa imepungaza kasi ya ukataji miti hivyo anawaalika wakazi na wananchi wa Mkoa wa Geita kutembelea katika Banda lake ili kuona aina mbalimbali za miti.

Mkurugenzi huyo pia ametaja aina za miti ya matunda ambayo pia anayo ni pamoja na ukwaju wenye Radha kama ya tende ambao pia unatiba ndani yake na mapera mekundu ya kilo Moja ambayo mbegu yake ni endelevu.

Wakati huo huo Mkurugenzi huyo ametoa ushauri Kwa wadau mbalimbali ambao wanaomba fedha Kwa ajili ya Mazingira kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwenye eneo lililokusudiwa na si kufanya ujanjaujanja kwani kufanya hivyo ni kurudisha nyuma harakati za Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambayo inahamasisha utunzaji wa Mazingira,kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini.