Na Mohamed Hamad, TimesMajira Online, Kiteto
MWENYEKITI wa Baraza la Ardhi Kata ya Bwawani Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Steven Tadayo amehukumiwa kulipa faini ya Sh.500,000 au kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) jela baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) pamoja na kifungu cha 15(2) vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007.
Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mossy Sasi amesema Mahakama iomeona kuwa mshtakiwa huyo ambaye ni Mwenyekiti ana kosa la kuomba na kupokea Rushwa huku mshtakiwa wa pili, Maiko Robert Lemabi ambaye alikuwa Katibu wa Baraza hilo akiachiwa huru.
Hakimu Sasi amesema kuwa, pia Mahakama hiyo imeamuru Mwenyekiti huyo wa Baraza kurejesha fedha za rushwa TAKUKURU ambazo alizipokea kwa njia mtandao wa simu.
Mapema Julai 2019, washtakiwa hao walimweleza mwananchi mmoja kuwa kufungua shauri anatakiwa kulipa kiasi cha Sh.10,000 ikiwa ni gharama ya Baraza na kumtaka awape Sh.20,000 (Rushwa) ndio wafungue shauri hilo.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua