Na Esther Macha,TimesmajiraOnline,Mbeya
IMEELEZWA kuwa katika kuweka mazingira mazuri kwa wananchi hususani wanawake wanaojishughulisha na ujasiriamali wa mazao, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imejenga Soko la kisasa la Mboga mboga ambalo litawezesha mazingira mazuri ambayo yatakuza uchumi pamoja na kuongeza mapato kwa halmashauri
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Februari 22,2025 ,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Rungwe na Diwani wa Kata ya Masoko,Mpokigwe Mwankuga amesema kwamba soko hilo litasaidia kuboresha mazingira mazuri ya uuzaji wa mboga mboga kwa wakulima hususani wanawake ambao wamekuwa wakijishughulisha na biashara hizo kwa muda mrefu.
“Halmashauri imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wananchi wake hasa wanawake kwani tumeweza kutengeneza soko la Mboga mboga ambapo tumetumia zaidi ya mil.180 katika ujenzi wa soko hilo ambapo wanawake wanaendelea kuuza mazao yao hapo hasa mboga mboga na tumendeelea kuhamasisha wananchi kilimo cha bustani na hata sasa tumepata wafadhili ambao watakutana na wizara ya maji kwa ajili ya kuchimba visima amesema.
Akielezea zaidi Mwenyekiti huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe smesema kuwa yapo maeneo machache ambapo kuna wafadhili wamejitokeza kupitia wizara ya Maji wanaenda kuchimba
visima ili watu waweze kujitengenezea bustani za mboga mboga .
Amesema kuwa soko hilo lipo Tandale ambalo halmashauri wakishirikiana na wafadhili ili kuhakikisha wananchi wanaotengeneza mazingira mazuri ya ufanyaji biashara za mboga mboga ambazo zitainua vipato vyao.
Aidha Mwankuga amesema kwa wilaya ya Rungwe kilimo wanachotegemea zaidi kwa wilaya ya Rungwe ni ndizi hivyo halmashauri imeendelea kuhamasisha kilimo bora na matumizi sahihi ya mbolea ili halmashauri iendelee kupata mapato kupitia ndizi .
Ukipita kila nyumba hutakosa ndizi lakini watalaam wetu bado wanaendelea kuhakikisha matumizi ya mbolea ili na sisi halmashauri tuendelee kupata mapato kupitia kilimo cha ndizi “amesema.
Atuganile Mwamboneke ni mkazi wa Kata ya Kiwira anayejishughulisha na uuzaji wa mboga katika soko la Tandale amesema kuwa uwepo wa soko hilo umemfanya kubadili maisha yake tofauti na awali.
“Kupitia biashara yangu hii ya mboga nashukuru Sana maisha yangu yamebadilika na halmashauri yetu ilivyotujengea soko hili imetufanya tupate hamasa zaidi kwani hivi sasa mboga mboga zetu hatupangi chini tena na hata mvua tumeikwepa tupo kwenye jengo zuri kama mnavyojua wilaya yetu hii msimu wote ni wa mvua,” amesema.
Amanyasye Juma amesema uwepo wa soko la mboga mboga itakuwa mkombozi Kwa wananchi wilayani humo hususani wanawake ambao kwa kiasi ndo wamekuwa wakijishughulisha na biashara hizo.
More Stories
Waislamu Mwanza wapokea Ramadhani kwa maandamano ya kidini
Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala,katiba na sheria yaridhishwa ujenzi soko Kariakoo
TRA Tanga yakusanya bil.178.3 kwa miezi sita