Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online,Rukwa
SERIKALI ya Mkoa wa Rukwa kwa kushirikiana na Kiwanda cha Alpha Tanganyika Flavour Ltd, imezindua Siku ya Uhamasishaji wa Kula Samaki mkoani hapa kwa lengo la kuongeza uelewa wa matumizi sahihi ya mchanganyiko wa vyakula vya makundi tofauti, yanayozalishwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huku msisitizo ukitolewa katika ulaji wa samaki.
Tafiti zinaonesha kuwa hali ya udumavu na utapiamlo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano mkoani hapa, imeshuka kutoka asilimia 56.3 ya mwaka 2016 hadi asilimia 47.9 ikiwa ni kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na mkoa katika kupambana na hali hiyo, ambayo inasababishwa na ulaji wa chakula cha aina moja hasa kundi la chakula cha wanga kuliko makundi mengine ya vyakula hasa protini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa wakati wa uzinduzi wa siku hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Dkt. Khalfan Haule amesema kuwa mkoa una vyanzo vingi vya uzalishaji wa samaki likiwemo Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa, Bwawa la Sundu, Bwawa la Kwela na mabwawa 328 yaliyopo katika maeneo mbalimbali ya mkoa.
Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya uzinduzi wa siku ya uhamasishaji wa ulaji samaki mkoani Rukwa, shughuli iliyohudhuriwa na uongozi wa wavuvi wa samaki Mkoa wa Rukwa, Maofisa Uvuvi wa Halmshauri pamoja na wadau wengine wa zao la samaki.
Amesema kwa mwaka 2018/19 na 2019/20 wastani wa tani 2,444.323 za samaki zimevuliwa katika vyanzo hivyo vya uvuvi na kuongeza kuwa asilimia 15 hadi 30 ya mwili wa samaki ni protini na mafuta ya samaki, yana omega 3 kuonesha kuwa ni mafuta bora na salama katika mwili wa binadamu, kwani hayasababishi magonjwa ya moyo kama yalivyo mafuta mengine.
“Ndugu Washiriki sisi kama serikali tutaendelea kushirikiana na mwekezaji Alpha Tanganyika Flavor Ltd katika kuhakikisha tunawahamasisha wananchi wa Mkoa wa Rukwa, kula samaki ili wawe na soko namba moja,” amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alpha Tanganyika Flavor, Aplha Nondo amesema pamoja na malengo mengine ya kuanzisha kiwanda hicho lakini lengo kuu ni kuwapatia wavuvi wa Ziwa Tanganyika soko la uhakika na hivyo kusababisha kutotumia muda mrefu kusafirisha samaki wao kwenda nchi jirani ya Zambia na matokeo yake kukosa muda wa kukaa na familia zao.
Akizungumza kwa niada ya wadau wa wavuvi wa samaki Diwani wa Kata ya Kabwe wilayani Nkasi, Asante Lubinsha ameushukuru uongozi wa Alpha Tanganyika Flavor Ltd, kwa kufungua kiwanda cha samaki mkoani hapa akiamini kuwa kitakuwa ni tegemeo kubwa kwa wavuvi na kutarajia kuwatoa katika hali ya umaskini na kuwasababisha kuwa katika hali ya kat.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi