September 30, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rukwa yaongeza kiwango upatikanaji wa maji

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online. Rukwa

MKOA wa Rukwa umeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi kutoka asilimia 40.1 iliyokuwepo mwaka 2016 hadi kufika asilimia 71.

Ongezeko hilo limechangiwa na miradi ya maji iliyotekelezwa na wataalamU wa Wizara ya Maji kwa kutumia utaratibu wa force account.

Akizungumzia ongezeko hilo Kaimu Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Boaz Matundali ameisema miradi ya maji 30 imekamilishwa maeneo ya vijijini na wananchi wanapata huduma.

“Miradi mingine 39 inaendelea na ipo katika hatua mbalimbali katika Wilaya za Sumbawanga, Kalambo na Nkasi,” meisema na kuongeza kuwa miradi hiyo inatekelezwa kupitia mpango wa Lipa kwa Matokeo (PforR), Lipa kwa Matokeo (PbR) na Uwezeshaji wa Mfuko wa Maji wa Taifa (NWF).

Ameongeza kuwa mkakati uliopo hivi sasa ni kuhakikisha wananchi katika idadi ya vijiji 124, wanapata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza kwa shughuli mbalimbali za kila siku.