March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ridhiwani ahimiza wenye uwezo kusaidia wengine

Na Mwandishi Wetu,TimesmajiraOline

WAUMINI wa kiislam wenye uwezo wamehimizwa kuzingatia maadili ya dini yao na kusaidia watu wa makundi mbali mbali hasa wakati wa mfungo wa Ramadhan ikiwa ni pamoja na kuliombea amani Taifa.

Nasaha hizo zilitolewa jana na waziri wa nchi ofisi ya Rais utumishi na utawala bora Mh.Ridhwani Kikwete wakati aliposhiriki hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na shirika la Bima la Zanzibar jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo iiyofanyika katika hoteli ya Johari Rotana ilihudhuriwa na viongozi,wadau wa shirika hilo na wafanya biashara ambapo walitumia fursa hiyo kuliombea Taifa huku wakisisitiza maadii kwa wafuasi wa imani zote.