Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania na Zambia zinajipanga kuhakikisha Reli ya Tazara inafanya kazi kwa uwezo wake wote na kuchochea uchumi wa nchi hizo mbili.
Akihutubia kwenye Bunge la Zambia Jana jioni, Rais Samia amesema kwa sasa reli hiyo inafanya kazi kwa asilimia nne tu ya uwezo wake jambo linalohitaji mabadiliko.
Reli ya Tazara ina uwezo wa kusafirisha kiasi cha tani za mizigo milioni tano (5,000,000) lakini kwa sasa kiasi cha tani laki moja na elfu themanini na nane (184,000) pekee ndizo zinazosafirishwa.
More Stories
Tanzania yajivunia ushirikiano kati yake na Kuwait
Mbunge Mavunde akabidhu mradi wa Shamba kwa wanawake wafanyabiashara wadogo Dodoma
Wasira aihakikishia Marekani uchaguzi nchini kuwa wa huru na haki