January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Mbeya: watumishi Tulia Trust endeeleni kuwa wazalendo

Na Esther Macha, Timesmajira majira,Online,Mbeya 

MKUU wa mkoa Mbeya ,Juma Homera amewataka watumishi wa Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Spika wa Bunge na Mbeya mjini  Dkt.Tulia Akson kuendelea kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa uaminifu na kutosikiliza maneno ya watu.

Homera amesema hayo alipotembelea banda la Taasisi ya Tulia Trust ambalo lipo kwenye viwanja vya John Mwakangale ajili ya kutoa elimu ya mikopo na Kazi zingine zinazofanywa na Taasisi hiyo kwenye maonesho ya wakulima Nanenane .

“Mnafanya kazi kubwa na asilimia kubwa nyie ni wabunifu wakubwa ndo maana mambo yanaenda,nimpongeze Mbunge wa jimbo la mbeya mjini kwakweli ameona dhamira kubwa ya kuwasaidia Wana mbeya ni kuanzisha Taasisi ambayo pengine itakuwa ni kuwasaidia wananchi na kweli imefanya kazi kubwa ambayo inaonekana,ninachowamba wafanyakazi mnaofanya kazi Tulia Trust endeeleni kuwa wazalendo yawezekana wakati mwingine watu wakawadanganya mbona mpo huko mnafanya nini Mungu atawalipa mnachofanya “amesema Homera.

Akielezea zaidi Homera amesema kuwa kumekuwa na kazi nyingi za ubunifu zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwemo tuzo kwa waandishi wa habari,ngoma za asili,pamoja na tuzo zingine,hivyo taasisi hiyo inazalisha ajira nyingi kwa vijana na ubunifu unaofanyika baadaye vijana wana uwezo kuanzisha shughuli zao binafsi kupitia Tulia Trust.

Aidha alipongeza bodi ya wakurugenzi inayoongozwa na Spika wa bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya,Dkt.Tulia Akson,nyie ni wabunifu sana na endeeleni kumsaidia mkurugenzi.

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa ameitaka Taasisi ya Tulia Trust kuweka taratibu za kutoa taarifa za tulia Trust Kwa mkuu wa mkoa wa mbeya kujua wamefanya nini na Serikali kuisemea Taasisi hiyo.

Joshua Edward ni Ofisa habari na mahusiano wa Taasisi ya Tulia Trust, amesema kazi kubwa ya Taasisi hiyo ni uwezeshaji Wananchi kiuchumi pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya.

Amesema zaidi ya asilimia 80 wanayohudumia ni wakulima na wafugaji na ili waweze kuwa wanufaika wa Tulia Trust ni lazima wawe kwenye vikundi vya watu watano.