Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya – Mhe. Juma Homera amezindua rasmi Kampeni ya Onja Unogewe inayoendeshwa na Benki ya NMB chini ya mwamvuli wa Teleza Kidijitali, inayowezesha malipo kwa njia ya NMB Lipa Mkonono (QR) kwa usalama wa pesa za wafanyabiashara na wanunuzi lengo likiwa kuhamasisha mhamo wa jamii kutoka kwenye matumizi ya pesa taslimu kwenda katika matumizi yasiyo ya pesa taslimu.
Akizungumza kuhusu kampeni ya NMB Onja Unogewe wakati wa uzinduzi katika viwanja vya stendi ya daladala ya Nane Nane jijini Mbeya, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Matawi ya NMB Bw.Donatus Richard alisema kuwa, licha ya Onja Unogewe kubeba dhana nzima ya suluhu za kifedha katika manunuzi na malipo, pia kampeni hiyo inawapa fahari wao kama benki katika kujenga mfumo Jumuishi wa masuala ya fedha kupitia mapinduzi ya kidijitali waliyoyafanyia uwekezaji mkubwa.
Donatus alibainisha kwamba, NMB inadhamiria kuhakikisha wafanyabiashara wanapata malipo yao moja kwa moja kwenye akaunti zao tena bila makato yoyote kwao wala wateja – kazi yao ni kuwapa wateja QR kuscan- Hii ni njia rahisi na salama kuhakikisha mahesabu hayapotei na hujihakikishia usalama wa fedha zao.
Moja ya faida anayopata mlipaji kupitia NMB Lipa Mkononi ni kuwa wigo mpana wa kulipia kidijitali na kunufaika na rejesho la hadi asilimia 10 katika malipo atakayofanya.
Mhe. Homera aliipongeza NMB kwa ubunifu na kuwaita ‘nyumba ya ubunifu’. Aidha, aliishukuru NMB kwa kuzindua kampeni hiyo jijini Mbeya, moja ya mikoa ya mpakani (Zambia na Malawi) ambayo inakabiliwa na matukio mengi ya wizi, ujambazi na upotevu wa pesa, huku akiwataka wafanya biashara na wajasiriamali wa Nyanda za Juu kuchangamkia fursa ya kutumia NMB Lipa Mkononi (QR) ili kukabiliana na changamoto hizo katika mauzo na manunuzi yao ya kila siku.
Vile vile, aliwaasa wana Mbeya – hasa watoa huduma za Bajaji, bodaboda, mama lishe, wauza maduka, wafanyabiashara na wajasiriamali, wanapaswa kuwa vinara katika kuchangamkia huduma hii.
Wekeni QR Code hizi madukani na sehemu zenu za biashara, ili kuwawezesha wateja kufanya malipo na kuepukana na mtukio hatarishi kwa fedha zao yanayoikabili jamii, hususani mikoa hio ya mipakani.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini