Fresha Kinasa,TimesMajiraOnline,Mara.
MKUU wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amewataka Watumishi wote wa serikali mkoani humo wawe tayari kupokea simu wanapopigiwa na Wananchi kutaka ufafanuzi na ufunguzi wa shida zao na pia wawatumikie Wananchi kwa moyo wa dhati.
Kanali Mtambi ameyasema hayo Januari 29, 2025 wakati akizungumza na Viongozi wa Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya Kiserikali Mkoani humo.
Kanali Mtambi amesema kuwa,Viongozi hao hawapaswi kujikweza pindi wanapotakiwa kutoa huduma kwa Wananchi kwani kufanya hivyo ni kurudisha Nyuma juhudi za serikali za kutatua changamoto za Wananchi kwa shabaha ya  kuchochea Kasi ya maendeleo.
“Watumishi muwe tayari kupokea simu na kusaidia Wananchi katika idara zenu, ninyi mlioko serikalini ni Watumishi wa watu acheni tabia ya majivuno muwe na moyo wa kuhudumia Wananchi wanapowafikia kwa upendo na moyo wote mkitambua kwamba dhamana mliyopewa. ni muhimu katika kusukuma mbele gurudumu la Maendeleo.”amesema Kanali Mtambi.
Pia, ametoa wito kwa Mashirika yote yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) Mkoani humo kuendelea kufanya kazi kwa kufuata Sheria na taratibu zote za nchi na Kutanguliza mbele uzalendo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwahudumia Wananchi wa Mkoa huo.
“Serikali ya Mkoa inatambua kwa dhati mchango wenu katika kuwahudumia Wananchi, baadhi ya miradi yenu mnayoifanya imeendelea Kusaidia kupunguza vitendo vya Ukatili wa Kijinsia ndani ya Mkoa. Niwaombe mzidi Kutanguliza mbele uzalendo na kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata Sheria na taratibu zote ambazo zinatakiwa.”amesema Kanali Evans Mtambi.
More Stories
Bungua mweusi anayeshambulia zao la kahawa aibuka Bukoba
DED mpya Mbeya DC ataka watumishi kuwatumikia wananchi
Rais Samia kuzindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2024 Toleo la 2023