Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Babati
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa sh.mil.470 kwa ajili ya ujenzi wa Shule Mpya ya Sarame inayojengwa katika Kijiji na Kata ya Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara.
Akizungumza na viongozi mbalimbali, wananchi wa Kata ya Magugu Wilayani Babati Mkoani humo, wakati wa kukagua shule hiyo Mkuu huyo alisema lengo la ziara yake ni kwenda kukagua na kuona hatua iliyofikia shule hiyo, ambapo tayari wanafunzi wamo Madarasani wakiendelea na masomo.
Kufuatia ujenzi huo Makongoro Nyerere amewapongeza viongozi mbalimbali akiwepo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo, Mbunge wa Jimbo hilo Daniel Sillo, madiwani, Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na wananchi wa Kijiji na Kata ya Magugu kwanushirikiano wao wankuhakikisha shule hiyo inakamilika Kwa wakati.
” Niwapongeze sana viongozi mbalimbali,wananchi Kwa kuonyeshanbidii za kuhakikisha mradi wa ujenzi wa shule Mpya ya Sekondari ya Sarame unakamilika na hatimaye sasa wanafunzi wanafunzi tunawaona wapo madarasa” amesema Makongoro.
Hata hivyo alisema katika hatua hiyo amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa sh.mil.470 Kwa ajili ya ujenzi wa Shule hiyo Mpya, hivyo ni vema wananchi wakaendelea kuunga mkono juhudi za Dkt.Samia Suluhu Hassan.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba