Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo amepokea tathimini ya utendaji kazi wa Wakandarasi wa Usafi na vikundi vya uzoaji taka ambapo tathimini imenyesha Wakandarasi wengi hawatekelezi majukumu yao ya kuondoa taka kwa wakati jambo linalosababisha kero kwa Wananchi.
RC Makalla amesema tathimini hiyo inaonyesha Kati ya Wakandarasi 256 wa Usafi Wanaofanya Usafi vizuri ni 73 sawa na Asilimia 28, Wanaofanya Usafi kwa wastani ni 171 sawa na Asilimia 67 na Wakandarasi ambao hawafai ni 12 sawa na Asilimia 5.
Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Wakandarasi na vikundi vya uzoaji taka kuhakikisha wanabadili mienendo yao kwa kufanya Usafi Kama mikataba inavyowaelekeza ili kufuta dosari walizoonyesha huku akielekeza Halmashauri kutozipatia Tena kazi kampuni zinazosuasua.
Akizungumza wakati wa kikao hicho RC Makalla amesema Kampeni ya Safisha Pendezesha Dar es salaam imepokelewaw vizuri na Wananchi na kuelekeza Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanadhibiti biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa huku akizitaka Taasisi kuyalinda maeneo yao yasivamiwe upya.
Aidha RC Makalla amemuelekeza Katibu tawala wa Mkoa huo kuwahamisha Watendaji wa Kata wanaonekana kuwakumbatia Wafanyabiashara Wanaofanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.
Maelekezo hayo ya RC Makalla yamepokelewa kwa mikono miwili na Wakandarasi, Vikundi vya Usafi na Wakuu wa Taasisi mbalimbali ambapo wameahidi kuyatekeleza kwa umakini mkubwa.
More Stories
CPA.Makalla :CCM kutumia 4R za Rais Samia katika uchaguzi Serikali za Mitaa
CCM kutumia 4R za Samia Uchaguzi Serikali za Mitaa
Dkt. Mpango awasilisha salam za Rais Samia mazisha Baba yake mzazi, Gavana Tutuba