Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema hajaridhishwa na utendaji kazi wa Mkandarasi wa Kampuni ya JASCO inayojenga Barabara ya Makongo juu Kutokana na mkandarasi huyo kutokuwa na uwezo wa kazi Jambo linalosababisha ujezi kusuasua kwa muda mrefu na kusababisha Kilio na adha kwa Wananchi.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea ujezi wa Barabara hiyo Kufuatia Kilio kikubwa Cha wakazi wa Makongo ambao wamelamikia Mradi kuchukuwa muda mrefu na Mchezo wa Mkandarasi kuonekana Eneo la kazi na kuweka Vifaa pindi wanapobaini Kuna Kiongozi anatembelea Barabara hiyo.
Kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa Mkandarasi huyo, RC Makalla amesema atafikisha Mapendekezo ya kuvunjwa kwa mkataba kwa Waziri wa Ujenzi Prof. Makame Mbarawa ili hatua zichukuliwe na kazi ikabidhiwe kwa Mkandarasi mwenye uwezo na Vifaa.
Aidha RC Makalla amewataka Wananchi wa Makongo kuwa watulivu wakati huu Serikali inachukuwa hatua.
Miongoni mwa kero na changamoto zilizotolewa na Wakazi hao mbele ya RC Makalla ni pamoja na Ubovu wa Barabara, Vumbi nyakati jua, Tope nyakati za mvua, Vifusi, Mawe na Kukosekana kwa Sehemu za kuingia kwa Wananchi.
Ujenzi wa Barabara ya Makongo yenye urefu wa Km 4.5 umeanza tokea mwaka 2019 kwa gharama ya Tsh Bilioni 9.1 lakini mpaka Sasa kazi iliyofanyika Ni Asilimia 60 Kutokana na sababu zinazoelezwa kuwa Mkandarasi Hana uwezo na Kutokana na madhaifu hayo Yamepelekea Wananchi kuchoshwa na kumuomba RC Makalla kuwasilisha Maombi ya kuvunjwa kwa mkataba.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu