December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla: Rais Samia amemaliza kero ya uhaba wa vyumba vya madarasa DSM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi Cha Shilingi bilioni 15.2 kwaajili ya Ujenzi wa Vyumba 743 vya Madarasa Jambo lililosaidia kupunguza kero ya uhaba wa Vyumba vya Madarasa.

RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa shule ya Kambangwa Wilaya ya Kinondoni kupitia Fedha zilizotolewa na IMF kwaajili ya UVIKO19.

Aidha RC Makalla amesema Mpaka Sasa Jumla ya Vyumba 570 Kati ya 743 vimekamilika na vilivyobaki vipo hatua za mwisho kukamilika ambapo mpaka Disemba 30 Majengo yote yatakuwa tayari kwaajili ya kupokea wanafunzi.

Hata hivyo RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Meya kusimamia kikamilifu Ujenzi wa Vyumba vikivyosalia ukamilike kabla ya Muda uliotolewa.

Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza Uongozi wa Shule ya Kambangwa kwa kukamilisha Ujenzi kwa wakati na kutoa wito kwa Wakuu wa Shule nyingine kuweka Mkazo kwenye Ujenzi huo.