Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais Samia Mgeni rasmi Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07.Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Utamaduni la kwanza kitaifa na Siku ya Kiswahili Duniani linalotaraji kuanza July 01-07 Jijini humo na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na Waandishi wa habari, RC Makalla amesema Tamasha Hilo litazinduliwa Julai 02 na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kwenye Uwanja wa Uhuru likihusisha Matembezi ya Utamaduni, Maonyesho ya vyakula vya asili na ngoma za asili.
Aidha RC Makalla amesema Julai 03 kutakuwa na Usiku wa Taarabu katika ufukwe wa Coco Beach ukihusisha burudani ya Mziki mwanana kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Patricia Hilary, Mzee Yusuph na wasanii na vikundi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson.
Hata hivyo RC Makalla amesema Julai 04 Kutakuwa na maandamano ya Amani kuhusu Lugha ya Kiswahili na Utoaji haki kutoka Temeke mwisho mpaka Uwanja wa Uhuru ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Katiba na sheria Dkt. Damas Ndumbaro.
RC Makalla amesema Julai 06 kutakuwa na kongamano la mchango wa lugha ya Kiswahili katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika likihusisha Viongozi kutoka ndani na nje ya Nchi.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Julai 07 Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Kiswahili Duniani ambayo itaadhimishwa kwa mara ya kwanza Dunia Ambapo ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa