Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo amepokea msaada wa Vifaa vya afya ikiwemo Vitanda na Meza vyenye thamani ya Shilingi Milioni 205 kutoka Jiji la Hamburg ya Ujerumani kupitia Taasisi ya The Free Hanseatic city Dada wa Jiji la Dar es salaam.
RC Makalla amesema kupatikana kwa Vifaa hivyo Ni Matokeo ya jitiada anazofanya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya mataifa mbalimbali.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo iliyofanyika hospital ya Wilaya ya Kigamboni, RC Makalla amesema msaada uliotolewa awali Ni Kontena 3 zenye Vitanda 108 na Meza 72 na awamu ya pili zitakuja Kontena 6 zenye vitanda 324, vitanda 151 vya wagonjwa mahututi na Meza 51.
Aidha RC Makalla Baada ya kupokea Vifaa hivyo amevikabidhi kwa Halmashauri za Dar es salaam ambapo Wilaya ya Kigamboni imepokea Vitanda 24 na kabati 16, Kinondoni vitanda 21 na kabati 14, Temeke vitanda 21 na kabati 14, Ilala vitanda 21 na kabati 14 na ubungo vitanda 21 na kabati 14.
Hata hivyo RC Makalla amesema msaada wa vitanda hivyo umekuja wakati muafaka na vitasaidia kupunguza Kero ya uhaba wa vitanda hospitalini.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja