December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla apokea mpango kazi wa shirikisho la bodaboda DSM

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla leo amepokea Mpango kazi wa shirikisho la Bodaboda Mkoani humo unaolenga kusajili idadi ya Waendesha Bodaboda, idadi ya Vituo na kuwaingiza kwenye mfumo rasmi ili kuondoa uholela katika Biashara hiyo.

Akipokea Mpango kazi huo, RC Makalla amesema mbali mpango huo kuweka Mazingira Bora ya Biashara pia utasaidia Serikali kupata Kukusanya mapato na kuimarisha Hali ya Ulinzi na usalama.

Hatua hiyo imekuja Baada ya Shirikisho la bodaboda kubaini kuwa Serikali imekuwa ikikosa Mapato zaidi ya Shilingi Bilioni 7 kila mwaka Kutokana Kukosekana kwa mpangilio mzuri wa uendeshaji wa Shughuli hiyo ambapo mapato ya Vituo yamekuwa yakiingia mifukoni mwa Wajanja na sio serikalini.

Kutokana Uholela huo shirikisho limeoma ni wakati muafaka kwa Serikali kuanza kupata mapato yatokanayo na kazi ya Bodaboda kwakuwa ni ajira rasmi.

Aidha RC Makalla amelielekeza shirikisho kumpatia ratiba ya siku watakazikwenda kuwasilisha Mpango kazi ngazi ya Wilaya ambapo amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuratibu jambo hilo kwa kuhakikisha linatekelezwa mpaka ngazi ya Mtaa.

Hata hivyo RC Makalla amepongeza hatua ya Shirikisho kupata mdau atakaetoa magari kwaajili ya kutoa huduma kwa Bodaboda watakaopatwa na majanga ya Ajali na misiba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la Bodaboda Mkoa wa Dar es salaam Said Chenja ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka Mazingira Bora ya Ufanyaji Biashara ya Bodaboda.