January 12, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Makalla ampongeza Rais Samia kwa kutatua kero ya barabara na mitaro Kata ya Mbweni

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ametembelea Ujenzi wa Barabara, Taa, Mitaro, Mifereji ya maji Kata ya Mbweni zenye urefu wa Km 14.5 inayogharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni 21 ambapo kukamilika kwake inakwenda kilio Cha muda mrefu Cha Wakazi wa Mbweni.

Akizungumza wakati wa Ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo, RC Makalla amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha zaidi ya Shilingi Bilioni 21 kwaajili ya Kata ya Mbweni Baada ya kupokea Kilio Cha Wakazi hao.

Miongoni mwa Barabara alizotembelea RC Makalla ni pamoja na Barabara ya Mbweni JKT yenye urefu wa Km 3.9 inayojengwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Nyanza road works kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.5 na Sasa Ujenzi upo Asilimia 50.

Aidha RC Makalla ametembelea Ujenzi wa Barabara ya Mkwajuni Mbweni yenye urefu wa Km 7 Chini ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya Kings Building kwa gharama ya Shilingi Bilioni 11.2 ambapo Ujenzi umefikia Asilimia 72.

Hata hivyo RC Makalla amekagua Ujenzi wa Barabara ya Mbweni kwa Somji yenye urefu wa Km 2.1 ambapo ametumia ziara hiyo kutoa wito kwa Wakandarasi kumaliza kazi kwa wakati ili waweze kujiwekea mazingira ya kupata kazi Mara kwa mara.

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Rais Samia kwa kutoa Shilingi Bilioni 9 kwaajili ya Ujenzi wa Mifereji ya maji kwenye maeneo yaliyokuwa yakikabiliwa na tatizo la mafuriko na maji kutwama kwenye Kata hiyo.