Na Heri Shaban, TimesMajira Online, Ilala
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala, amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ni sehemu hatarishi kufanya Biashara sababu ya kubeba magonjwa mbalimbali .
Mkuu wa Mkoa Amos Makala, amesema hayo katika Oparesheni ya safisha na Pendezesha Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Usafi eneo la hospitali ya Taifa Muhimbili Kata ya Upanga Magharibi .
“Eneo hili sio rasmi kufanya Biashara ni eneo hatarishi watu kuchukua magonjwa kwenda kwa Jamii, Mitaani, magonjwa hatarishi ” amesema Makala .
Mkuu wa Mkoa Makala amesema sehemu hiyo ambayo waliokuwa aakitumia wafanya Biashara sio sehemu rafiki kufanya Biashara ,Daladala pia zinatakiwa kushusha na kuondoka .
Amesema kuanzia leo anaweka Kambi eneo hilo atakuwa anakuja kila wakati atasimamia masaa 24 hivyo amewataka Wafanyabiashara kuondoka sio sehemu Salama .
“Nakuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kuanzia Leo simamia eneo hili sio rafiki kufanya Biashara wanapofanya Biashara wanabeba na magonjwa hatarishi aliwataka hospitali ya Taifa Muhimbili kuyalinda maeneo hayo Kipindupindu ni uchafu nawaomba Wananchi wa Ilala kuyapendezesha maeneo haya ” amesema
Katika hatua nyingine amepongeza KAMPUNI ya Usafi ya Kajenjele ambayo inashiriki kampeni za Pendezesha Dar Esalaam na kuunga mkono juhudi za kufanya Usafi Kila wakati eneo ambalo Serikali inazindua kampeni hizo Mkurugenzi wa Kajenjele anaacha Shughuli zake anajumuika pamoja ikiwemo kutoa magari ya usafi .
Wakati huohuo walijitoeza Wadau wa usafi akiwemo Diwani Mstaafu wa Upanga Magharibi Godwini Mbaga amesema atakabidhi shilingi milioni 1 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuunga mkono kampeni hiyo kabambe ambapo Mkuu wa Mkoa Amos Makala alimweleza Mbaga kuwa apeleke Ofisini kwa Kaimu Katibu Tawala Mkoa atampa pesa hiyo na kupewa risiti Maalum .
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua