January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mkuu wa Mkoa azitaka TARURA, TANROADS kuwashirikisha wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha Bodi ya Barabara ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe walipata taarifa za maendeleo ya ujenzi wa barabara mkoani humo kutoka Tanroad na Tarura jijini Dodoma.Mahenge amezitaka TARURA na TANROADS kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika kwa kupata maoni na ushauri wao kabla ya kuanza ujenzi wa barabara na
madaraja katika maeneo yao ili kujenga miradi imara inayozingatia jiongrafia na historia ya eneo husika.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Happiness Mgalula akisoma ajenda za kikao hicho.
Spika wa Bunge, ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akitoa hoja kuhusu umuhimu wa Miji midogo kama Kibaigwa kutengewa na Tanroads fedha za ujenzi wa barabara na kupanua maeneo ya kuegesha magari yakiwemo malori ili kupanua wigo wa kibiashara na kuongeza ajira kwa vijana katika eneo hilo. Ndugai pia ni mjumbe wa bodi hiyo.
Mhandisi wa Barabara wa Tanroads, Clement Ngirwa akielezea katika kikao hicho, kuhusu utaratibu wa kupandisha hadhi barabara na majukumu ya
Kamati ya Kitaifa ya Kupanga Barabara katika Hadhi Stashiki.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Sezaria Makota akichangia hoja wakati wa kikao hicho. Kuhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Dk. Fatuma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda.
Mbunge wa Mvumi, Livingstone Lusinde akichangia hoja akitaka uwepo utaratibu wa barabara za jamii nazo kutengea fedha kwa ajili ya
matengenezo.