November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC CHALAMILA:Ashukuru Serikali ya Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar kwa usimamizi wa viwanda vya ndani

Na Penina Malundo, timesmajira

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amemshukuru serikali ya Tanzania na Zanzibar chini ya Rais Dkt Samia Suluhu na Dkt Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa ambapo wameweza kusimamia viwanda vya ndani ambavyo vinazalisha bidhaa nyingi zinazouzwa katika masoko ya ndani na nje.

Akizungumzia hayo jana Julai wakati akitrmbelea maonesho ya Sabasaba ya Kimataifa 2023 katika viwanja vya Mwl Julius Nyerere Temeke Jijini Dar es Salaam amesema ni jukumu kubwa ambalo watumishi wa Serikali wanapaswa kuliendeleza kwa kiasi kikubwa ili mwisho wa siku Tanzania iweze kujulikana kimataifa.

Aidha RC Chalamila amefurahishwa na bidhaa mbalimbali zinazouzwa na wafanyabishara wa aina mbalimbali, wadogo, wa kati na wakubwa huku akiwataka watanzania ambao bado hawajafika katika viwanja hivyo kuja kujipatia bidhaa na kujionea fursa anuai kwani maonesho ya 47 yameboreshwa sana.

Aidha Chalamila amesema kupitia wafanyabishara walioko katika viwanja hivyo vya maonesho yanaleta picha ya Kimataifa, Kitaifa na ngazi ya chini kabisa ya Wajasiriamali ambao ni wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali ya Rais Dkt Samia.

RC Chalamila amewataka wafanyabishara kuendelea kufanya biashara na kuwahakikishia ulinzi na usalama upo wa kutosha pia muda wa kufanya biashara umeongezwa hadi saa 2 usiku.

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANTRADE Latifa Khamis amemshukuru Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila kwa kufanya ziara hiyo na usimamizi wake katika Kipindi chote cha maandalizi ya maonesho.

Pia amesema ulinzi na usalama umeimarika hata hivyo ujio wake umewafariji wananchi na wafanyabishara wa ndani na nje kwa kuwa wanaona Serikali inavyounga mkono maonesho hayo.

“Wafanyabishara wameendelea kufanya biashara vizuri, hivyo ametoa rai kwa wananchi walioko majumbani kuja kujipatia bidhaa mbalimbali katika maonesho hayo ya Kimataifa ya 47,”amesema.