Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert Chalamila amezindua kampeni ya kujenga hosteli za wanafunzi wa kike mkoa Dar es Salaam na kuwataka Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wajiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa kuwa Taifa linawategemea.
Mkuu wa mkoa Albert Chalamila alisema hayo wakati kuzindua kampeni kabambe ya kujenga hosteli za Wanafunzi wa kike wa mkoa huo na kuwakabidhi hundi za shilingi milioni 100 kwa mkoa huo kwa ajili ya kuanzia ujenzi ambapo kila kila Wilaya walipewa hundi ya milioni 20.
“Mkoa Dar es Salaam tunaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya wanafunzi wa kike kuwajengea hosteli tunathamini sana watoto wa kike na Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ,Rais wetu siku yake ya kuzaliwa January 27 mwaka huu “alisema Chalamila
Mkuu wa mkoa Chalamila amesema katika mkoa huo hali ya matokeo sio mazuri lakini wakianza kujenga hosteli za wanafunzi wa kike hali itakuwa nzuri katika sekta ya elimu kwa kuongeza ufaulu hivyo mkakati wao ni kuanza na wanafunzi wa kike
Alisema hosteli hizo za wanafunzi zina faida kubwa kuliko kuwa acha nyumbani wanafunzi kwani mwanafunzi wa kike anatakiwa awe na mazingira bora ya kumlinda sababu amebeba kizazi cha kesho hivyo wakiwekeza kwa kizazi cha sasa watapata kizazi bora cha Taifa letu.
Aidha katika hatua nyingine Chalamila aliwataka walimu wa shule za Msingi na Sekondari wajiamini wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani wao ni watu muhimu na Taifa linawategemea ambapo alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo ,walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa kusimamia vizuri fedha za serikali za sekta ya elimu kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na shule mpya za kisasa.
Aliwataka walimu wa mkoa huo kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu na wawe walimu wema waliobeba ndoto za wanafunzi .
Aliwataka Walimu wafanye kazi na kujiamini wataonekana kutokana na kazi yao kufanya kwa weledi wasirudi nyuma wachanganue mambo wenyewe kwa wenyewe kwani elimu sio cheo.
Aliagiza kila Halmashauri za mkoa huo kufanya harambee kwa kuwashirikisha wadau kwa ajili ya kupata fedha za kujenga Hosteli za wanafunzi wa kike waweze kusoma katika mazingira bora na kuandaa Ramani ya mchoro ya ujenzi ya hosteli hizo huku wakiweka mpango kazi endelevu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alitumia fursa hiyo kuwapongeza walimu wa mkoa huo wa elimu msingi na sekondari kwa kazi nzuri waliofanya sekta ya Elimu kupelekea wanafunzi kufanya vizuri kitaaluma pamoja na sekta ya michezo .
Pia aliwapongeza walimu kwa kusimamia vizuri fedha za Serikali katika ujenzi wa shule za Sekondari na shule za msingi kwani walimu wamekuwa watu muhimu katika Taifa ili sio wa kuwazalau .
Katibu Tawala mkoa Dar es Salaam Rehema Madenge aliwataka walimu waendelee kudumisha nidhani na kufanya kazi kwa weledi kwa kuwa kioo na kuwataka wafute misingi bora ya kazi.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa