January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC Chalamila ataja chimbuko la Panya Road

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert Chalamila, amesema chimbuko la makundi ya vijana wa Panya Road Chanika na Zingiziwa hivyo amewaasa wazazi wenye watoto hao kuwalea watoto wao katika misingi mema wasiingie katika makundi hatarishi .

Mkuu wa mkoa Chalamila, amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Chanika na Zingiziwa Jimbo la Ukonga wilayani Ilala wakati wa kusikiliza kero za wananchi na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo.

“Chimbuko la makundi hatarishi, panya Road Chanika na Zingiziwa naomba Wazazi muwalehe watoto wenu katika misingi bora kitendo cha kunyanyua panga na nyundo mnadai wanajeshi sasa hivi kimeisha mwisho wake umefika kwani ukimchekea nyani utavuna mabua na aliyeuwa kwa upanga utauwawa kwa upanga mimi nasema atajua baadae” alisema Chalamila.

Chalamila alisema hivi karibuni kiongozi mwandamizi wa Panya Road, aliuwawa Vingunguti kundi la vijana hatarishi panya Road wakaenda kulipiza kisasi katika mkoa wangu vitendo hivyo basi vimefika mwisho Wazazi muwalehe watoto wenu katika misingi mema wasiingie katika makundi hatarishi.

Katika hatua nyingine alisema Wazazi wa Zingiziwa na chanika wameshindwa kuwalea watoto katika misingi bora katika mkoa wake wa Dar es salaam inaongoza kwa madanguro watoto wadogo wanaingia katika Biashara hiyo wamiliki wamepewa vibari lakini wanatumia vibaya Taifa letu la Tanzania lazima tukemee Madanguro na mmomonyoko wa maadili kwa vijana.

Akizungumzia sekta ya ardhi alisema baadhi ya viongozi wa Serikali sio waminifu hawana msaada katika sekta ya ardhi baadae wanakuwa kero kwa watanzania nimefanya ziara jimbo hili la UKONGA sitaki ubabaishaji na unafiki badala yake aliwataka wawe wakweli.

Aliwataka wananchi wa Zingiziwa na chanika kuwa na imani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM ambapo Rais Samia amefanya mambo makubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya,na miundombinu ya Barabara.

Aidha aliwataka wananchi kuwa wakweli wasiogope kiongozi wowote awe wa Serikali au Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kama awezi kuwajibika asemwe hadharani

Akizungumzia mafuriko alisema katika mkoa wake amna mafuriko hivyo aliwataka wananchi waliojenga mabondeni wachukue hatua za kuondoka mara moja maeneo hatarishi sio salama kwa makazi ya watu ,aliwambia Wananchi wakitaka kununua kiwanja wanunue wakati wa masika na wakitaka kununua kiwanja katika maeneo ya fukwe za Bahari wanunue wajati wa Bahari kujaa