May 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rc Chalamila aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Charles Hilary

Na Mwandishi wetu, Timesmajira

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Mei 13, 2025 ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu na Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Charles Hilary Jijini Dar es Salaam.

RC Chalamila wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Charles Hilary katika Kanisa la mtakatifu Batholomayo Anglikan, Dayosisi ya Ubungo ameongoza harambee maalum kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa Kanisa hilo ikiwa ni Sadaka lakini pia kumuenzi marehemu kwa kuwa wakati wa uhai wake alikuwa mtu wa kujitoa sana katika kanisa.

Aidha mwili wa Charles Hilary umeagwa na Viongozi wa Serikali, Mabalozi, Taasisi mbalimbali, wawakishi kutoka vyombo vya habari na watu wengine mashuhuri.

Mwisho mwili wa Charles Hilary unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea Zanzibar kwa ajili ya maziko.