Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Tabora
MKUU wa Mkoa wa Tabora Dkt.Philemon Sengati ametoa siku 56 kwa Mkandarasi Mzinga Holding Company Limited kuhakikisha wanakamilisha jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Mji wa Nzega.
Amesema licha ujenzi wa jengo hilo kufikia asilimia 92 bado shughuli umaliziaji wake unasuasua na kuwafanya watumishi wa Halmashauri hiyo waliohamia kurundikana katika vyumba vilivyokamilika.
Dkt.Sengati ametoa agizo hilo jana wakati ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika Halmashauri hiyo ikiwemo Ofisi hiyo na Bweni la Wanafunzi katika Sekondari Bulende.
“Mimi kwa kweli sijafurahishwa na kasi ya ujenzi …nimekuja hapa kuna maeneo kazi zimesimama …nawaagiza chapeni kazi usiku na mchana ili jengo lote limekamika katika muda mliomba kuongezewa” amewaagiza.
Dkt.Sengati amesema Mkandarasi kuchewesha kazi ni kutaisababishia Serikali kutumia gharama za ziada,jambo ambalo halikubaliki.
Amemtaka Mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana na kwa uzalendo wa hali ya juu ili kuhakikisha kazi zilizobaki zinakamilika katika muda aliopatiwa wa Juni 30 mwaka huu na kuongeza kuwa kinyume cha hapo itabidi Serikali kuchukua hatua.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega Philemon Magesa amesema kuwa Mkandarasi wa jengo hilo ambalo linagharimu zaidi shilingi zaidi shilingi bilioni 5 ambapo alipaswa kuwa amekamilisha mwishoni mwa Aprili mwaka huu.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa