December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

RC ataka ushirikishwaji scout katika matukio DSM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemuelekeza Afisa Elimu wa Mkoa huo kuhakikisha kuanzia Sasa Vijana wa Scout wanashirikishwa Katika shughuli mbalimbali na sio kusubiri yatokee Matukio ya Majanga, Mikutano, ugeni wa Viongozi au Misiba ndipo umuhimu wao unaonekana.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati alipotembelewa ofisini kwake na Kamishina wa Scout Dar es salaam alieambatana na Watendaji wa TAKUKURU na kukabidhiwa Kitabu Cha Mwongozo wa mafunzo kwa wawezeshaji kufundisha Vijana wa Scout kuhusu kuzuia na kupambana na Rushwa.