December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais samia ziarani nchini China

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Viongozi wakuu wa nchi za Afrika na China 🇨🇳 mkutano unaotarajiwa kuaanza tarehe 4-6
Katika ziara hiyo nchini China 🇨🇳

Atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Atahutubia ufunguzi wa mkutano wa FOCAC.

Atafanya mazungumzo na Rais China, Mhe. Xi Jinping na kushuhudia uwekaji saini wa Hati za Makubaliano ya Uboreshaji wa Reli ya TAZARA.

Atakutana na makampuni na wawekezaji kutoka China ili kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.