Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua rasmi Jengo la Kitega Uchumi (Safina House) la Kanisa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), katika Viwanja vya Kanisa Kuu la Roho Mtakatifu Jijini Dodoma leo
August 15, 2023.
Akizindua jengo hilo, Rais Dkt. Samia alisema amefurahishwa na kukamilika kwa jengo hilo ambalo limechukua takribani miaka sita.
“Nilikuwa kila nikipita naona mavyuma hapa kwenye hili jengo nikawa nasema litakamilika lini, toka nimelifahamu ni mavyuma tu, leo tumshukuru Mungu jengo limekamilika lakini pia limepewa jina zuri sana Safina, Safina ambayo Baba Askofu ameielezea vizuri ilimbeba Nabii Nuhu na mizigo yake yote ya wanyama na ndege”
“Nataka niwaambie kwamba ile Meli ilitua Dar es salaam na ndio maana wanyama wote wale wakaenda Serengeti , Ngorongoro na maeneo mengine na kutupa sifa Tanzania ya kuwa na wanyama wazuri na bora na Watu wanatoka Ulimwenguni kote kuja kuwaangalia, ile Meli Ilitua Dar es salaam”
“Pia jina hili linaashiria mambo makubwa kama ilivyowavusha wale, ilivushe Kanisa Anglikana lakini pia iivushe Tanzania salama, jengo hili ni la kitega uchumi kuashiri kukua kwa uchumi wa Kanisa la Anglikana, Serikali imefurahishwa kukamilika kwa mradi huu ambao utachangia kiuchumi na kijamii”
Aidha Rais Dkt. Samia aliwaagiza TRA kuendelea kukusanya Kodi kama kawaida
“Jengo hili limechukua miaka sita, huduma zitakazotolewa ndani ya jengo hili sasa tunakaribia kuzipata na nimefurahishwa kuona nembo ya NMB imetanda hapo mbele na kwamba NMB ni Wapangaji wakubwa humu ndani lakini pia TRA wapo humu ndani na mambo ya kodi yametajwa humu lakini sio kwasababu umepangishwa usamehe kodi hapana kodi yetu ikusanywe kama kawaida”
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba