Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekuwa miongoni mwa viongozi bora wa kuigwa duniani katika Maonesho ya Dunia yanayoendelea ya Dubai 2020 Expo.
Hayo yamesemwa leo tarehe 14 Desemba, 2021 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) alipotembelea banda la wanawake “Women’s Pavilion” katika maonesho hayo yanayoendelea Dubai.
Masanja amempongeza Rais Samia kwa kuongoza maendeleo ya nchi ya Tanzania na hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine duniani.
Aidha, amewahimiza Watanzania kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Samia katika jitihada za kuleta maendeleo ya nchi ya Tanzania.
More Stories
Kanisa la Shincheonji la Yesu nchini Ufaransa lakanusha ripoti ya Le Parisie
Vyombo vya ulinzi na usalama Mbeya,Benki kuu kushirikiana kutatua changamoto za utapeli mtandaoni
Polisi Mbeya kuimarisha ulinzi kuelekea sikukuu ya Pasaka