Na Mwandishi wetu, Timesmajiraonline,Dodoma
KUANZIA Agosti, 2024 Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, atakuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Nafasi hii itaiwezesha Tanzania kuratibu, kusimamia na kuongoza majadiliano na maamuzi yote yanayohusu masuala ya siasa, ulinzi na usalama.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma, jana.
Aidha, nafasi hii itaimarisha ushawishi wake katika ukanda wa SADC katika masuala haya hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Waasisi wa SADC walioshiriki kwa hali na mali katika harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto