January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azindua shule 302, ataka wazazi kuwapeleka watoto shule

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan leo October 15,2023 amefungua Shule ya Msingi Imbele na shule ya Sekondari Mwanamwema kwa Niaba ya Shule Mpya 302 Zilizojengwa Nchi Nzima kupitia program ya BOOST na SEQUIP ambapo ametoa wito kwa Wazazi kuwapeleka wototo Shule.

Rais Dkt, Samia amezindua Shule hizo wakati wa Ziara ya Kikazi Mkoani Singida ambapo pia amesema Serikali imedhamiria kuboresha elimu na kumuandaa mtoto kuanzia awali mpaka elimu ya juu.