January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia azawadia wananchi wa Zambia

Na Jackline Martin, TimesmajiraOnline,Zambia

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameamua kutenga hekta 20 za ardhi katika
Bandari Kavu eneo la Kwala mkoani Pwani ikiwa ni zawadi kwa wananchi wa Zambia.

Rais Samia alitoa zawadi hiyo kwa wananchi wa Zambia jana wakati akihutubia katika maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa Zambia yaliyofanyika katika viwanja vya Ikulu.

Alisema katika utekelezaji wa kuwapa wananchi kipaumbele katika
maendeleo, anawazawadi wananchi wa Zambia ardhi katika eneo hilo,
kwani yeye na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ni waumini wa
kuwawezesha wananchi katika maendeleo ya kiuchumi.

Wakiongelea mgawanyo wa raslimali, Rais Samia alisema msisitizo ni
kila mwananchi kunufaika. “Kaulimbiu ya ‘Kuchapusha Maendeleo ya
Kitaifa kupitia Ugawanaji wa Raslimali imekuja wakati muafaka si to kwa Zambia, lakini pia kwa nchi nyingine za Afrika ikiwemo Tanzania.”

Rais Samia alisema siku ya Uhuru unaosherehekewa ni kwasababu waasisi wa Mataifa hayo mawili, (Keneth Kaunda na Julius Nyerere) waliamini, wakapambania walichoamini na kuandaa mipango ya utekelezaji.

Wakati huo huo nchi hizo mbili zimedhamiria kujenga bomba jipya la
gesi kutoka Dar es Salaam hadi Zambia, pia wamepanga kuimarisha bomba la mafuta TAZAMA pamoja na reli ya TAZARA.

Rais Samia anaendelea na ziara ya siku 3 Jamhuri ya Zambia kwa mwaliko wa Rais Hichilema ikiwa na malengo ya kuimarisha uhusiano wa kindugu pamoja na kiuchumi.