November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia awezesha ujenzi Barabara ya Vingunguti

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan, ametoa shilingi milioni 44,380,000.00 kwa ajili ya kipande cha Barabara ya Butihama kilichojengwa kwa kiwango cha zege Ili kurahisisha mawasiliano ya Barabara Barakuda na Vingunguti .

Akizungumza katika ufunguzi wa barabara hiyo Meya Omary Kumbilamoto alisema Barabara ya Kizala yenye urefu wa mita 80 imejengwa kwa fedha za Serikali kufuatia kuwa kero mda mrefu na kukata mawasiliano ya Barabara na kupelekea Wananchi waeneo hilo kuishi kama kisiwa.

“Rais Samia Suluhu Hassan amesikia kilio cha Mtaa Butihama Barabara ya Kizala ametoa fedha kipande cha mita 80 kimejengwa kwa kiwango cha zege kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ya Barabara ” alisema Kumbilamoto .

Meya Kumbilamoto amewataka Wananchi wa Vingunguti kuweka itikadi za vyama vya siasa pembeni Ili wadumidhe Maendeleo katika kuisaidia Serikali na kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekekezaji wa Ilani .

Meya Kumbilamoto alisema mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka ni bilioni 81 na Halmashauri hiyo ina matumizi makubwa ya fedha imelazimika kuomba fedha za Rais katika kutatua kero hiyo ya Barabara .

Aidha alisema Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA watajenga mitalo ya Barabara hiyo .

Pia alisema katika kilima hicho kilichojengwa kwa kiwango cha zege zitafungwa taa za kisasa kwa ajili Usalama nyakati za usiku magari yakipita eneo hilo .

Akizungumzia kero ya maji Kata ya Vingunguti alisema Wananchi waliokosa maji ya Dawasa amewataka waandike barua kwa Meneja wa DAWASA Tabata waweze kuunganishiwa maji ya Bomba .

Wakati huohuo alisema ataomba Rais Samia Suluhu Hassan, asikie kilio cha pili ajenge Daraja la Barakuda Msimbazi kutokea Vingunguti ambapo Daraja hilo likijengwa Vingunguti itakuwa ya kisasa.