Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais Samia Suluhu Hassan akibadilishana mawazo na Rais wa Brazil, Lula Da Silva mara baada ya kukamilika kwa mkutano wa 15 wa Jumuiya ya BRICS.
BRICS ni Jumuiya kubwa ya pili ya kiuchumi duniani, ikiwakilisha idadi ya watu wanaokaribia bilioni 3.5. Jumuiya hii inaundwa na nchi 5 waanzilishi ambazo ni Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini.

Mkutano huu umetangaza rasmi nchi nyingine 6 zitajiunga na kuwa wanachama rasmi wa jumuiya hii kuanzia January 2024. Nchi hizo ni Argentina, Saudi Arabia, Egypt, UAE, Iran na Ethiopia.
Mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Jumuiya hii inayokua kwa kasi yanaiongezea Tanzania wigo wa ushirikiano na fursa za kiuchumi.
More Stories
Mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa waongezeka hadi asilimia 9.0
Wizara ya Nishati yajivunia jitihada katika kulinda haki, usawa na kuwawezesha wanawake
Mpina,Maganga kuendelea kuwafichua viongozi mafisadi na wabadhilifu