Na Mwandishi wetu,timesmajira
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ametembelea ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora ambapo alipata nafasi ya kusaini vitabu vya wageni, kukutana na kufanya mazungumzo na kamati ya siasa ya mkoa huo.
Pamoja na mambo mengine Mwenyekiti wa CCM Taifa alipokea taarifa ya mwenendo wa uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea na kujadiliana masuala mbalimbali yenye ustawi na CCM na wananchi wa Tabora kwa ujumla.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Shaka Hamdu Shaka amesema Rais Samia  yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku tatu aliyoianza Mei 17,2022 na kuhitimishi 19,2022 kwa kuwahutubia wananchi wa mkoa wa Tabora katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Â
Awali Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Mwakasubi akimkaribisha Ndg Samia Suluhu Hassan amueleza kuwa Chama Cha Mapinduzi mkoani Tabora na wananchi kwa ujumla wanaridhishwa na utendaji wa serikali anayoiongoza katika kuimarisha utoaji huduma, ujenzi wa miundombinu na ukuzaji wa uchumi kwa wananchi mkoani humo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
“Nimekuwa mwanachama wa chama hiki na kiongozi kwa miaka 25 lakini tukio la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutembelea ofisi za chama chetu na kuzungumza na viongozi wake hili ni tukio la kwanza kwa mkoa wa Tabora. Haya ni mahusiano mazuri baina ya chama na serikali, tunakushukuru sana na tunakukaribisha Tabora.” amesema Mwakasubi.
More Stories
Mashirikisho yaunga mkono azimio mkutano mkuu CCM
Watumishi wa Mahakama waonywa
CCM ilivyotambua mchango wa wanahabari Mkutano Mkuu Maalum