Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo ameshiriki kwa heshima kubwa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC-Organ Troika Summit) uliofanyika Harare, Zimbabwe.
Mkutano huu ni jukwaa muhimu kwa majadiliano kuhusu amani, usalama, na ulinzi katika kanda ya Kusini mwa Afrika.
Katika mkutano huu, Rais Dkt. Samia amesisitiza kwa nguvu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika masuala ya ulinzi na usalama, ili kuhakikisha ustawi na amani kwa wananchi wa nchi wanachama wa SADC.
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kupokea uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, ikiashiria kuendelea kwa Tanzania kuwa na nafasi muhimu na yenye kuheshimika katika masuala ya siasa, ulinzi, na usalama barani Afrika.
More Stories
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato
Wambura asikitishwa na makundi CCM Nyakato