December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia amesikiliza kilio cha wakazi wa Ngorongoro

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwemo za elimu na afya zilizokuwa zimesitishwa katika Tarafa ya Ngorongoro.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa Agosti 23, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi akizungumza na wananchi wa kata 11 zilizopo Tarafa ya Ngorongoro, akiwasilisha maagizo ya Rais aliyewatuma kuwasilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku 5 wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.

Aidha amesema Rais ameagiza uchaguzi katika tarafa hiyo kwa kutumia mipaka ya zamani, ufanyike kama unavyofanyika maeneo mengine nchini.