Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
RAIS Samia Suluhu Hassan amekabidhi cheti cha pongezi kwa ushiriki wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwenye tamasha la Kizimkazi Festival 2024, wakati wa Hafla ya chakula cha usiku iliyofanyika Ikulu ndogo Kizimkazi Zanzibar.
Cheti hicho cha pongezi kimepokelewa kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, Nassoro Juma Kuji, na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Jully Bede Lyimo – Mkuu wa kitengo cha Maendeleo ya Biashara pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi Amina R. Salum ambaye ni Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa Ruaha.
TANAPA, kwa dhati na unyenyekevu mkubwa tumepokea na kuthamini heshima hii kubwa kutoka kwa Dkt Samia Suluhu Hassan.
More Stories
Kituo cha afya Kisiwa cha Rukuba chafungiwa umeme jua kurahisisha huduma
Kapinga:Wakandarasi wasimamiwe kutekeleza miradi ya nishati kwa wakati
Rungwe yajenga soko kukuza uchumi kwa wananchi