November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aendelea kuinua sekta ya Anga

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuhakikisha Sekta ya Anga inafanyiwa maboresho makubwa kwa ununuzi wa ndege, kuboresha Viwanja vya Ndege na ununuzi wa rada 4 za kuongozea ndege ambapo Mamlaka ya usafiri wa Anga (TCAA) wameendelea kuwa askari namba moja wa kuhakikisha kwamba malengo hayo ya serikali yanatokea nchini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Abdallah Komba katika marthon iliyoandaliwa na Mamlaka ya usafiri wa Anga (TCAA) za Km 5 mpaka Km 10 ikiwa ni katika muendelezo wa kuadhimisha miaka 20 ya Mamlaka hiyo.

“RAIS samia anaipa kipaumbele eneo la Anga ili kuruhusu Tanzania iweze kufikika kupitia Anga , kazi kubwa inafanyika Katina kuboresha viwanja vya ndege na tayari Mamlaka hii inaendelea kutoa huduma kwenye viwanja 15 katika Taifa letu”

“Shirika letu la ndege limeendelea kuimarishwa mpaka sasa tunazo ndege takribani 13 zilizonunuliwa na serikali yetu kwaajili ya kuchochea ukuaji wa Sekta ya Anga Tanzania” Amesema

Komba amesema uboreshwaji wa Sekta ya Anga, Reli na miundombinu katika Sekta ya maji unalenga kuifanya Tanzania ifikike kwa mazingira tofauti tofauti nchini.

“Mamlaka ya usafiri wa Anga nyie ndiyo askari namba moja mnaotegemea na Rais Samia kuifanya Tanzania ifikike kwenye Kona zote za Dunia”

“Ktokana na umadhubuti na umakini walionao TCAA pamoja na ufanisi wao, viwanja vya ndege nchini vitaendelea kuwa imara wakati wote na anga litaendelea kuwa salama ambapo itapelekea kupokea Makampuni mengi ya ndege kutoka Duniani kuja Tanzania.” Ameongeza

Komba amewapongeza TCAA kwa kuhakikisha kunakua na chuo cha mafunzo ya mda mfupi ya wataalamu wa Sekta ya usafiri wa Anga na kuwataka kuendelea kuimarisha chuo hicho lakini pia kuhakikisha kunakuwepo na wataalamu wa kutosha ili kuendelea kuzalisha wataalamu wengi zaidi ambao wataendelea kusaidia katika ukuaji wa Sekta ya Anga Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari ametoa wito kwa Wana anga wote, watumishi na watanzania kwa ujumla kujali afya zao , kuzingatia mlo na kufanya mazoezi kwani mazoezi ni tiba na ni sehemu ya afya ambayo itasaidia kuepuka magonjwa nyemelezi na kuhatarisha maisha.

Mbali na hayo amesema leo wanatimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake ambapo watakua na mkutano mkubwa wa Wana anga huku mgeni rasmi akiwa ni waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ambapo watazungumzia walipotoka tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo na wanapokwenda kwa miaka ijayo.

Naye Lugalo Masomola kutoka LATRA ambaye katika mbio hizo amekimbia Km 5 amesema mashindano yalikua mazuri na atajitahidi kufanya vizuri zaidi kwa mashindano yajayo.

Matukio mbalimbali katika picha