Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Rais Samia Suluhu Hassan amechaguliwa na jarida maarufu duniani Times la Marekani kuwa ni mmoja wa watu wa 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa
Mwaka 2022.
Rais Samia ambaye aliingia madarakani mwaka jana kufuatia kifo cha ghafla cha Rais John Pombe Magufuli amechaguliwa kwenye kundi la viongozi wenye ushawishi mkubwa kwa sasa duniani.
Wengine kwenye kundi hilo ni pamoja na Rais wa Marekani Joe Biden, Putin wa Urusi, Zelensky wa Ukraine, Xi Jinping wa China, Rais wa Umoja you a Ulaya Ursula Von der Leyen,kansela wa Ujerumani Olaf Scholz,Letitia James ambaye ni mwanasheria mkuu wa New York kutoka Chama cha Democratic pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Aby Ahmed.
Akimuelezea rais Samia baada ya uteuzi huo, Rais wa zamani wa Liberia Helen Sirleaf Johnson alisema toka achukue madaraka amefanya mabadiliko makubwa.
“Milango imefunguliwa kwa ajili ya majadiliano na maridhiano miongoni mwa mahasimu wa kisiasa, hatua zimepigwa katika kujenga upya imani ndani ya mfumo wa kidemokrasia,juhudi zimefanyika katika kuongeza uhuru wa habari na wanawake na wasichana hivi sasa wanaye mtu mpya mustakhbal wa maisha yao yaani mtu wa kuigwa)role model)” alisema Rais hiyo zamani wa Liberia.
Amesema September 21 mwaka jana Rais Samia alikuwa Rais wa tano wa kike kutoka Afrika kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutoa hotuba nzito.
“ alisimama katika mahali(podium) ambapo mimi nilisimama miaka 15 iliyopita nikiwa Rais wa kwanza wa kike kutoka Afrika kulihutubia Baraza hilo” alisema na kuongeza..
“Rais Samia alisema hapa na mnukuu’ nikiwa Rais wa kwanza wa kike nchini mwangu, nabeba mzigo mzito wa matarajio ya kuleta usawa wa jinsia’mwisho wa kumnukuu.Wakati anazungumza maneno haya mazito kabisa nilijikuta nikifikiri na kuwaza nguvu za mabega ya viongozi wa kike kubeba dhima hiyo na kwa umbali gani wataweza kutoa matokeo chanya” alisema Bi Sirleaf ambaye pia ni mshindi tuzo ya amani ya Nobel.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato