January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Rais Samia aagiza mkoa wa Manyara kutenga makazi ya muda ya waliokumbwa na mafuriko

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameiagiza serikali yake kuhakikisha Serikali ya Mkoa na Kitengo cha Maafa cha Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka makazi ya muda ya watu ambao makazi yao yamesombwa na maji kwa lengo la kuwastiri wananchi hao wilayani Hanang, mkoani Manyara, haswa katika vijiji vya Katesh, Jorodom, Ganana, Dumbeta, Gendabi, Sarijandu, Arukushay na Sebasi.

Kwa taarifa za awali nyumba na mifugo imeathirika sana huku idadi za kaya zilizoathirika ni 1,150, idadi ya watu walioathirika hadi sasa ni 5,600 na pia ikikadiriwa takriban ekari 750 za mashamba zimeharibika.